19 Machi 2011 - 20:30

Mwandishi wa Kiislamu wa Algeria Boualem Sansal ameshinda Tuzo ya Amani ya Frankurt Ujerumani.

mwandishi huyo mwenye umri w miaka 62 ameshinda tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kueneza uhuru wa kusema, uhuru wa kueleza itikadi na dini na kuikosoa serikali ya Algeria.Sansal ambaye alipokea tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika Frankfurt amesema kuwa wananchi wanataka uhuru wa kijamii, na uhuru huo haupasi kubanwa na tawala za kidikteta, zenye misimamo mikali au madola yanayounga mkono mfumo wa kibepari.Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani pia imetoa taarifa ikitangza kuwa tuzo hiyo imetolewa si kwa sababu ya athari na maandishi ya Boualem Sansal pekee bali pia kutokana na jitihada zake za kutetea uhuru na demokrasia.Boualem Sansal ni miongoni mwa wanafikra wachache mno wa Algeria ambaye wamekuwa wakikosoa waziwazi hali ya kijamii na kisiasa inayotawala nchi hiyo.Tuzo ya Amani ya Maonyesho ya Vitabu ya Frankurt ni tuzo ya kimataifa yenye thamani ya yuro elfu 25 na ilianzishwa mwaka 1949 na kutolewa kwa mara ya kwana mwaka